BAMAKO, Mali.
WATU wenye silaha wamewaua takriban watu 23 na kujeruhi 12 kufuatia shambulio lililofanywa katika kijiji kimoja katikati mwa Mali, maafisa walisema mwishoni mwa wiki.
Sidi Mohamed El Bechir, Gavana wa Jimbo la Bandiagara ambako shambulio hilo lilifanyika, alisema watu
wasiojulikana waliua dazeni za watu Ijumaa iliyopita na kuchoma moto nyumba kadhaa katika Kijiji cha Yarou.
“Washambuliaji walikaa kijijini hapo hadi saa 7:00 mchana na kuteketeza sehemu ya kijiji, kuvunja maduka
na kuchukua ng’ombe wa wanakijiji,” alisema Amadou Lougue, Rais wa Shirika la Vijana la kieneo siku ya
Jumapili iliyopita.
BBC.