Watu saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 700 kujeruhiwa hivi leo kutokana na tetemeko kubwa la ardhi nchini Taiwan, ambalo limeharibu majengo kadhaa na kusababisha kutolewa kwa onyo la sunami hadi katika mataifa jirani ya Japan na Ufilipino. Maafisa wanasema tetemeko hilo ndilo kubwa kabisa kuwahi kukikumba kisiwa hicho kwa miongo mingi na wameonya matetemeko mengine madogo madogo yanaweza kuendelea kutokea katika siku zijazo.