WATU wawili wamefikishwa mahakamani nchini Uganda, kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Brenda Nantongo Wamala, mtoto wa Waziri wa uchukuzi nchini humo, Jenerali Edward Katumba Wamala, mapema mwaka huu.
Watuhumiwa hao ni dereva wa bodaboda, mwenye umri wa miaka 38 na daktari wa miti shamba mwenye umri wa miaka 46, ambao kwa pamoja wanahusishwa na mauaji hayo ya Brenda na dereva wa Waziri, Haruna Kayondo.
Jenerali Wamala alinusurika katika shambulizi hilo na kuambulia majeraha madogo katika mkono wake, ambapo taarifa zinasema tayari amerejea kazini kuendelea na majukumu yake.
Terehe 1, mwezi huu, gari la Waziri Wamala, lilimiminiwa risasi na watu waliokuwa kwenye pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili, ambapo inadaiwa washambuliaji walikusudia kumuua Waziri Wamala.
Picha Waziri Wamala akiwa na bintiye enzi za uhai wake.