KOCHA mpya wa Barcelone,Xavi Hernandez, leo Novemba 08, 2021, anatarajia kuanza kazi rasmi kukinoa kikosi hicho cha Camp Nou, ambapo ametia saini mkataba kuwa kocha wa timu hiyo hadi mwaka 2024
Kiungo huyo wa zamani wa Barcelona, mwishoni mwa wiki alitangazwa kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha Ronald Koeman, aliyetimuliwa kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo.
Xavi leo anatarajia kuanza kusimamia mazoezi ya kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata katika michuano mbalimbali.
Kocha Xavi aliwasili katika kikosi hicho jana na kukamilisha utaratibu wa kuanza kuinoa timu hiyo ambapo alitia saini mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2014.
Taarifa kutoka katika mtandao wa klabu ya Barcelona, ilisema kocha huyo ataanza kazi rasmi leo na mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Espanyol itakayopigwa Novemba 20, mwaka huu baada ya kumalizika mechi za Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hata hivyo taarifa hiyo ilisema kuwa Barcelona inakabiliwa na wachezaji majeruhi wakiwemo Eric Garcia na Nico Gonzalez ambao wamepata matatizo ya misuli katika mechi dhidi ya Celta Vigo waliotoka sare ya mabao 3-3.
Vilevile Ansu Fati anaendelea na matibabu baada ya kuumia katika mchezo huo na hali yake inazidi kuimarika.
BARCELONA, Hispania