KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya haki za matangazo na kampuni ya Azam TV, wenye thamani ya sh. bilioni 34.8 kwa miaka 10.
Katibu Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria, Haji Mfikirwa, amesema mkataba huo utakuwa na marejea kadri ya muda unavyokwenda.
Amesema hiyo ni historia kwa klabu za Afrika Mashariki na Kati.
Uchambuzi wa mwandishi wa UhuruOnline, Abdul Dunia, unaeleza kuwa kwa makubaliano hayo, Yanga ni mabilionea.
Anasema Bonus kama Yanga itamaliza katika nafasi mbili za juu za ligi ni sh. bilioni 3 na kuendelea.
Kila mwezi watakuwa wakipata kiasi cha sh. milioni 200 na kuendelea.
Marejeo ya mkataba kama uongezwe, upungue ama uvunjwe yatafanyika kila baada ya miaka mitano
Kadhalika, mkataba huo utahusisha kurusha mechi za kimataifa, kirafiki, mazoezi na mahojiano binafsi kwa viongozi, wachezaji na benchi la ufundi la Yanga.
Na Abdul Dunia