KLABU ya Yanga imenogewa na biashara na wachezaji kutoka DR Congo na sasa iko kwenye hatua za mwisho kumsaini winga fundi kutoka Union Maniema, Basiala Agee (25).
Kwenye Ligi ya Congo sasa Basiala amefanikiwa kufunga mabao matano na kutoa asisti tano huku akiwa amekosa mechi mbili za mwisho kutokana na maaamuzi viongozi wakijiandaa kumruhusu aondoke kuanza maisha mapya na Mabingwa wa nchi, Yanga SC.