BAADA ya miaka 21, staa wa aliyemaliza muda wake katika kikosi cha Barcelona, Lionel Messi, anaondoka na ameshacheza mechi 778 huku akipachika mabao 672, na mkongwe huyu hatarudi tena katika kikosi hicho cha Camp Nou.
Uongozi wa Barcelona, tayari ulishatangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba wameamua kuachana na staa huyo kutokana na kushindwa kumwongeza mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika tangu Juni, mwaka huu.
Messi, mwenye umri wa miaka 34, alikuwa mchezaji huru tangu Juni 30, mwaka huu kufuatia mkataba wake wa awali kumalizika na kwamba uongozi hautamwongeza mkataba mpya mfungaji huyu wa muda wote wa Barcelona.
Katika makala haya tuangalie baadhi ya matukio yaliyomfanya staa huyu kuweka rekodi ya aina yake ndani ya Barcelona na kwamba ataendelea kukumbukwa na mashabiki wa kikosi hicho kwa kipindi kirefu kutokana na mafanikio aliyoipa hadi anaondoka.
BAO LA KWANZA BARCELONA
Ilikuwa Mei Mosi, mwaka 2005, akiwa na umri wa miaka 17, aliingia dimbani akitokea bechi ambapo alichukua nafasi ya Samuel Eto’o, raia huyo wa Argentina akivalia jezi namba 30.
Katika mechi hiyo Barcelona ilikuwa ikiikabili Albacete, ambapo Messi alifanikiwa kufunga bao pekee katika dakika ya 90 akipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Ronaldinho aliyeruka katikati ya mabeki wawili na Messi kuukwamisha mpira wavuni moja kwa moja.
2007 EL CLASICO ‘HATTRICK’
Baada ya miaka miwili, mashabiki wa soka walionekana kuanza kumfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji huyo aliyekuwa na umri mdogo zaidi kikosini.
Katika mechi iliyowakutanisha na watani wao wa jadi Real Madrid, Messi alionyesha uwezo mkubwa wa kucheza kandanda safi ambapo alifunga bao la kwanza mapema mechi hiyo ikichezwa Camp Nou.
B a a d a y e alipachika bao la pili na kuisawazishishia timu yake iliyotanguliwa mabao mawili na matokeo yalisomeka 2-2.
Sergio Ramos alifunga bao la tatu kwa Real Madrid wakati huo wenyeji wakiwa pungufu, lakini dakika tatu kabla ya mpira kumalizika, Messi alipachika bao la tatu na kuingia katika rekodi ya kufunga ‘hat-trick’ ya kwanza ambapo timu yake iliondoka na pointi moja.
BAO LA MAAJABU DHIDI YA GETAFE
Baada ya mwezi mmoja kupita mechi ya El Clasico, Messi alifunga bao la maajabu ambalo lilifananishwa na aliyewahi kufunga Diego Maradona.
Ilikuwa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Ligi ya Hispania, dhidi ya Getafe, Messi alipewa pasi na Xavi katika eneo la katikati ya uwanja na alianza kutambaa nao kupitia upande wa kushoto, aliwapita wachezaji watano na kufumua shuti kali lililojaa wavuni moja kwa moja.
Messi baada ya kufunga bao hilo, aliingia katika orodha ya mchezaji wa Barcelona kufunga bao bora zaidi katika historia ya klabu na siku iliyofuata aliteka vichwa vya habari vya magazeti yote Hispania ambapo vilisomeka ‘Messidona’.
BAO LA KICHWA DHIDI YA MANCHESTER UNITED
Mabao ya kichwa kwa Messi sio chaguo la kwanza lakini ameshafunga mabao 20 pekee kwa kichwa, katika kipindi chote a l i c h o c h e z a ndani ya Barcelona.
L a k i n i bao ambalo l i l i o n e k a n a k u m t a m b u l i s h a zaidi kwa kufunga kwa kichwa, a l i f u n g a m w a k a 2009, katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiikabili timu ya Manchester United wakati huo ikiwa chini ya Kocha Sir Alex Ferguson.
Katika mechi hiyo Messi alifunga bao la kichwa akiruka juu futi saba na kujaa wavuni moja kwa moja ambapo alipokea krosi murua kutoka kwa Xavi.
BAO ALILOFUNGA WEMBLEY
Miaka miwili baadaye Barcelona ilikutana kwa mara nyingine na Manchester United, katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa katika Uwanja wa Wembley.
Messi hakufunga bao katika mechi nane za mwisho za Ligi Kuu ya Hispania, lakini katika ardhi ya Uingereza alionyesha kiwango cha hali ya juu.
Alifunga bao katika umbali wa yadi 25, baada ya kufumua shuti kali lililomshinda kudaka kipa Van der Sar na kubeba taji hilo kwa mara ya tatu.
MABAO MATANO DHIDI YA BAYER LIVERKUSEN
M e s s i alikuwa mchezaji wa kwanza wa Barcelona, kufunga mabao matano katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. B a r c e l o n a mechi ya k w a n z a walipoteza u g e n i n i k w a m a b a o 3-1 dhidi ya Bayer Liverkusen, na hivyo walihitaji ushindi zaidi ili kusonga mbele katika michuano hiyo.
Hata hivyo katika mechi hiyo Messi alifanikiwa kufunga mabao matano pekeyake na alikaririwa akisema hakuamini kile kilichotokea.
“Sina uhakika na kilichotokea kwani hata mimi sikutegemea, lakini straika yoyote anaweza kufanya hivyo,”.
ALIVUNJA REKODI YA GERD MULLER
Awali mchezaji Gerd Muller aliweka rekodi ya aina yake ya kufunga mabao 85, ambayo ilikaa muda mrefu zaidi bila kuvunjwa.
Lakini mwaka 2012, Messi aliivunja rekodi hiyo kwa kupachika wavuni mabao 91 katika mechi 69 alizocheza Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.
REKODI YA KUFUNGA LIGI KUU
Baada ya muda mrefu kupita, Messi aliweka rekodi nyingine ya kufunga mabao katika Ligi Kuu ya Hispania katika mechi dhidi ya Sevilla wakishinda mabao 5-1, alifi kisha idadi ya mabao sawa na Telmo Zarra aliyewahi kufunga mabao 251.
MABAO 500
Kama mchezaji akitaka kufikisha idadi ya mabao 500 katika timu moja, anahitajika kuwa mtulivu kwa kiasi kikubwa, Messi alifanya hivyo kwa kifukisha idadi hiyo ya mabao Aprili mwaka 2017.
KUFIKISHA MABAO 650
Hakuna aliyewahi kuota kwamba anaweza kufikisha idadi ya mabao 650 katika timu moja, lakini Messi alifikisha kwa juhudi zake binafsi.
Messi alifikisha idadi hiyo ya mabao mwanzoni mwa mwaka na kuipiku rekodi ya Pele aliyewahi kuiweka ya kufunga mabao 643.
Messi anaondoka Barcelona, akiwa na rekodi mpya baada ya kufunga mabao 672.
BARCELONA, Hispania