BUNGE limemtia hatiani Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima na kuamuru asihudhurie mikutano miwili ya bunge huku ikishauri chama chake husika kumchukulia hatua na vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza kauli zake.
Aidha, Bunge limemtia hatiani Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa na kumsimamisha kuhudhuria mikutano miwili ya bunge na kuondolewa kwenye uwakilishi wa bunge la Afrika (PAP).
Wajumbe hao walikuwa kwenye kamati ya maadili hivyo wamejadiliwa na wajumbe wenzao hadi kufikia uamuzi huo.
Selina Mathew, Dodoma



























