BINGWA katika masuala ya Ubadhilifu Kudhibiti Rushwa na Ufisadi, Shakibu Nsekela, amesema RIPOTI ya Kimataifa ya mwaka 2021 iliyotolewa na Taasisi ya taaluma ya kudhibiti Ufisadi Duniani (ACFC), inasema asilimia 5 ya mapato yanapotea kwa ufisadi kwenye taasisi zote za umma na binafsi.
Pia amesema unapotokea ufisadi taasisi hutumia gharama kubwa namna ya kufanya uchunguzi ukaguzi na pesa zilizochukuliwa kuzirudisha.
Nsekela amebainisha hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya siku Tano ya kuwajengea uwezo taasisi za umma na binafsi kuweza kudhibiti ufisadi katika maeneo yao.
Pia ameeleza kuwa katika utendaji kazi wao wamebaini kuwa, ufisadi unaosikika ni ule unaosikika au kujulikana na ufisadi mwingi hazigunduliki au wahusika kuelewana wenywe kwa wenyewe na kupotea.
“Unapotokea ufisadi taasisi hutumia gharama kubwa namna kwa kufanya uchunguzi ukaguzi na pesa zilizochukuliwa kuzirudisha inakuwa ni changamoto,”amesema.
Amesema kutokana na hali hiyo wameona mwarobaini wa kudhibiti ufisadi ni kuzuia ufisadi usitoke na ndio lengo kuu la mafunzo hayo.
Nsekela amesema kazi yao kubwa ni kuwajengea uwezo taasisi za umma na binafsi juu ya dalili za ufisadi namna gani zinatokea na jinsi ya kuthibiti ufisadi.
Naye wakili wa kujitegemea na Muhadhiri wa sheria mwandamizi, Dk. Clement Mashamba, ameeleza kuwa tatizo la ufisadi ni kubwa kwani watu wengi wanaamini kuwa ili uweze kuwa tajiri lazima ufanye ufisadi lakini pia zipo sababu za kusababisha tatizo hilo liwepo.
“Ufisadi unatokea kwa sababu kuna fursa za kufanya hivyo watu wanashinikizio na tatu kuwepo kwa mianya na fursa watu kufanya ufisadi,”amesema.
Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakivunja sheria na taratibu zilizowekwa kutokana na usimamizi ni mdogo hali inayopelekea ufisadi.
Dk. Masamba amesema wanaangalia kuendelea upya sheria ili ziweze kubana mianya ya ufisadi na mambo yanayoibuka mapya katika ufisadi kwani sasa ufisadi upo kwenye njia za kidigitali mitandao.
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa idara ya uchunguzi wa ndani Benki ya Taifa ya biashara NBC, Meshaki Shashi, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yanawaweka pamoja ili nawao kwa umoja wao waende kupambambana na ufisadi katika maeneo ya taasisi za umma na binafsi.
Mwakilishi huyo amesisitiza kuwa “ufisadi ni tatizo kubwa nchini na si kana kwamba lipo kwenye mabenki tu sehemu zote lakini kwenye benki yangu ya NBC ipo kama taasisi na ndio maana tupo hapa katika kuhakikisha kupeana uwezo kudhibiti uhalifu huu.” Amesema Meshaki
Na Happiness Mtweve, Dodoma



























