Saturday, July 4, 2026
[gtranslate]
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result

DK. MWIGULU ASIFU BENKI YA DUNIA KUWEKEZA SH. TRILIONI 12 ZA MIRADI

Sh. Bilioni 1.167>> Zitatekeleza miradi mitano ya maendeleo ikiwemo ya sekta ya elimu na umeme

admin by admin
October 29, 2021
in Habari Kitaifa
0
DK. MWIGULU ASIFU BENKI YA DUNIA KUWEKEZA SH. TRILIONI 12 ZA MIRADI

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuwekeza zaidi ya sh. trilioni 12 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo  nchini.

Dk. Mwigulu ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dk. Hafez Ghanem, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), iliyofanyika kwa njia ya mtandao, Jijini Dar es Salaam.

“Miongoni mwa fedha hizo ni pamoja na kiasi cha dola za marekani bilioni 1.167 zilizotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mitano ya maendeleo ikiwemo ya sekta ya elimu, miundombinu, umeme na Tanzania ya Kidijitali kwa lengo la kuchochea uchumi jumuishi na kupambana na umasikini,” amesema.

Dk. Mwigulu  amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kinahusisha utekelezaji wa miradi 26 ya maendeleo inayopata fedha kupitia dirisha la mikopo nafuu (IDA) la Benki ya Dunia yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.502.

Amesema kuwa miradi 21 kati ya hiyo ni ya kitaifa yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 4.804 na miradi 5 ni ya kikanda yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 0.698, mpaka sasa kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.932 kimetolewa na benki hiyo sawa na asilimia 35 ya fedha zote.

Waziri huyo amezungumzia hatua zinazochukuliwa na serikali kupambana na athari za kiuchumi na kijamii zilizosababishwa na ugonjwa wa UVIKO-19,  amesema  serikali imeandaa mpango wa mwaka mmoja wa kukabiliana na athari za ugonjwa huo utakaogharimu shilingi trilioni 3.62

“Tayari serikali imepokea dola za Kimarekani milioni 567.25 sawa na takribani sh.trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiwa ni mkopo nafuu kwa ajili ya kunusuru maisha ya watu pamoja na uchumi wa nchi kutokana na athari hizo za UVIKO-19,” amesema.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo na Meneja Uendeshaji wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Preeti Arora, wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), iliyofanyika kwa njia ya mtandao, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa fedha hizo zimeelekezwa kutatua changamoto za athari za UVIKO-19 kwenye sekta ya utalii, kunusuru kaya masikini, maji, elimu na Afya upande wa Tanzania Bara na Zanzibar na akatoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuunga mkono jitihada hizo za Serikali ili kusisimua uchumi wa nchi.

Amesema hivi karibuni Serikali inatarajia kukamilisha mazungumzo na Benki ya Dunia kwa ajili ya kupata fedha za miradi miwili ikiwemo mradi wa kuboresha masuala ya ardhi na kuongeza msukumo wa kujifunza kupitia elimu ya msingi.

Kuhusu suala la wanafunzi wanaoacha masomo, Dkt. Nchemba amemwambia Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem kwamba changamoto ni kubwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa wanafunzi (wasichana na wavulana) 198,620 waliacha masomo katika shule za msingi wakati wanafunzi 113,484 wa shule za sekondari waliacha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo vifo, utoro, utovu wa nidhamu na ujauzito.

Akizungumza katika Mkutano huo, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayezisimamia nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dk. Hafez Ghanem, aliipongeza Tanzania kwa hatua mbalimbali inazozichukua katika kusimamia uchumi na maendeleo ya wananchi wake.

Ameahidi kuwa, Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia itakutana hivi karibuni kujadili maombi mbalimbali ya fedha yaliyotolewa na Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi  ya maendeleo ili fedha hizo zipatikane kwa wakati.

Dk. Ghanem ameshauri masuala kadhaa yafanyiwe kazi na Serikali ikiwemo kuongeza jitihada ya kuyasaidia makundi maalumu yakiwemo ya vijana na wanawake ili waweze kujengewa uwezo wa kiuchumi pamoja na kukuza ajira.

Amesema suala la wasichana wanaopata ujauzito wakiwa shuleni wajengewe mazingira ya kuendelea na masomo baada ya kujifungua, suala ambalo Dk. Mwigulu alimweleza kuwa, serikali inalifanyia kazi na kuangalia utaratibu utakaofaa zaidi kushughulikia suala hilo.

Aidha, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, amepongeza utaratibu mzuri ulioanzishwa na serikali wa kuimarisha na kuishirikisha sekta binafsi katika kutekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati ya maendeleo kupitia mpango wa ushirikiano wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.

Na Mwandishi Maalumu

Previous Post

RAIS SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO WA 26 WA UMOJA WA MATAIFA

Next Post

VINARA MATUKIO YA UJAMBAZI MBARONI

admin

admin

Next Post
MGANGA WA KIENYEJI AKUTWA NA HATIA YA KUBAKA

VINARA MATUKIO YA UJAMBAZI MBARONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Instagram Youtube Twitter Facebook

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • autohenriquesevale.pt
  • best casino
  • Best online casino
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • Casino No Deposit Bonus
  • Casino UK
  • casino1
  • casino2
  • casino3
  • casino4
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • gambling platform
  • gambling platforms
  • Gry
  • gry hazardowe
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • mew casino
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • Nasi Partnerzy
  • new casino
  • niam.cl
  • non gamstop casinos
  • Nos partenaires
  • OM cc
  • Online Casino
  • Online Kasyno
  • Our Partners
  • Partners
  • Post
  • Pozyczki
  • Prestamos
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • sanodelucas.cl
  • SIASA
  • Slots
  • Sports
  • test
  • The best new online casino
  • The best online casino and sportsbook
  • UK Casino
  • Uncategorized
  • Unsere Partner
  • veterinariarepublica.cl
  • wildbeauty.cl
  • www.kuss.cl
  • Микрокредит
  • Наши Партнеры

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved