Sunday, July 5, 2026
[gtranslate]
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result

DK. MWINYI ATAKA WANASHERIA Z’BAR KULETA MABADILIKO

Sh. Bilioni 16.8>>> Gharama za ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Zanzibar

admin by admin
January 10, 2022
in Habari Kitaifa
0
DK. MWINYI ATAKA WANASHERIA Z’BAR KULETA MABADILIKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwepo wataalamu wa sheria wenye ujuzi ni muhimu katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Dk.Mwinyi amesema hayo katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu, lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema juhudi za serikali za kuimarisha majengo na upatikanaji  wa vifaa, hazina budi kuambatana na utoaji wa mafunzo, ambapo wafanyakazi wa kada ya sheria watapata fursa ya kushiriki ndani na nje ya nchi.

Alisema wataalamu wa sheria wanapaswa kuishauri serikali masuala muhimu ya maendeleo, ikiwemo uandaaji wa mikataba na taasisi za kimataifa.

Alieleza kukamilika ujenzi wa jengo hilo ni hatua muhimu katika kutekeleza azma ya serikali ya kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi katika utumishi wa umma, kama ilivyobainisha katika mkakati wa mabadiliko katika Utumishi wa Umma wa 2010.

Dk. Mwinyi alisema kwa miaka mingi Mhimili wa Mahakama ulikuwa ukikabiliwa na changamoto  ya ufinyu wa nafasi na uchakavu wa majengo, huku mengi yakiwa yamerithiwa kutoka kwa wakoloni, ikiwemo Jengo la Mahakam Kuu lililopo Vuga, Jijini Zanzibar.

Alisema serikali itaendelea na dhamira ya kujenga majengo ya kisasa na kuweka  vifaa vya kufanyia kazi vinavyoendana na mabadiliko, mahitaji ya wakati uliopo.

Alitoa wito kwa watumishi wa umma kutunza vifaa na mejengo yaliyopo katika maeneo yote ya kazi kwa kutambua kuwa ni mali ya wananchi.

Dk. Mwinyi aliagiza uongozi wa Mahakama kuendelea kulitunza jengo lililopo Vuga, huku akisisitiza azma ya serikali ya kulifanya eneo la Mji Mkongwe kutumika kwa shughuli za utalii.

Alimshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya saba Dk. Ali Mohamed Shein kwa maono na kuja na wazo la ujenzi wa jengo jipya la Mahakama, na kusema uamuzi wake ulikuwa ni wa kimaendeleo.

Akigusia changamoto zinazoihusu Mahakama, aliagiza uongozi wa Mahakama  kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoukabili mhimili huo.

Alisema ujenzi wa jengo hilo ni mikakati ya serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, na kubainisha uwezo wa serikali wa kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia rasilimali zake wenyewe.

“Ujenzi wake umezingatia mahitaji ya wananchi kwa namna tofauti, ikiwemo upatikanaji wa huduma za benki na watu wenye mahitaji maalumu…..ni imani yangu kuwa watendaji watakaofanyakazi katika jengo hili watafanyakazi kwa kuzingatia uwajibikaji na uadilifu”, alisema.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kama ishara ya Ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar,Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wengine ni Viongozi mbali mbali wakishuhudia tukio hilo.

Kaimu Jaji Jaji Mkuu Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, alisema ujenzi wa jengo hilo umetokana na jengo la Mahakama Kuu lililopo Vuga kuwa na changamoto nyingi, ikiwemo ufinyu wa Ofisi, kutokuwa rafiki kwa jamii ya watu wenye ulemavu na mfumo wa Tehama.

Alisema wakati wa kipindi cha vikao vya  Mahakama ya Rufani, baadhi ya Majaji hulazimika kuchukua likizo ili kupisha Majaji wa Mahakama ya Rufani kuendelea na majukumu yao.

Alisema changamoto kubwa inayokabili Mahakama katika usikilizaji wa kesi za udhalilishaji ni mashahidi  kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi, huku baadhi ya nyakati wahusika wa kesi hizo wakibainika kufunga ndoa.

Kaimu Jaji Ramadhan, alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kufikiria uwezekano wa kujenga jengo jipya la Mahakama Kisiwani Pemba, kufuatilia lile liopo hivi sasa katika eneo la Kichungwani   Chakechake kuwa katika mazingira yasiofikika kirahisi kutokana na changamoto ya ukuaji  wa mji.

Aidha, Waziri wa Nchi, Katiba, Sheria, Utumishi wa Uma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman alisisitiza  haja ya watendaji wa Mahakama kuwajibika ipasavyo kiutendaji ili kwenda sambamba na mazingira halisi ya jengo hilo.

Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema ujenzi wa jengo hilo ni kielelezo cha dhamira ya serikali katika kuhakikisha mhimili wa Mahakama unawezeshwa, hivyo akaiomba serikali kuendelea na uwezeshaji huo hadi ngazi za chini.

Alisema jengo hilo ni zuri na linatoa matumaini katika utoaji wa haki, hivyo akabainisha mtihani unaowakabili watendaji wa mhimili huo katika kuhakikisha matumaini ya wananchi yanafikiwa, kuendana na mahitaji ya ujenzi wa Uchumi wa Buluu.

MUONEKANO wa jengo jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu, lililozinduliwa na Rais Dk.Mwinyi ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
(Picha na Ikulu)

Aliwataka Majaji na Mahakimu kujiwekea utaratibu wa kuwajibika na kuhakikisha jengo hilo linaendana na kasi ya maendeleo ya Zanzibar, huku akiahidi Mahakama Kuu ya Tanzania kuendelea kushirikiana kikamilifu na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Mapema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kai Bashiru Mbarouk  alisema Jengo hilo la Mahakama Kuu lililopo Tunguu  limegharimu sh. bilioni 16.8, ambapo fedha zote hizo kwa asilimia mia moja  zinatoka katika mfuko wa  serikali.

Alisema jengo hilo lililojengwa na Kampuni ya Advent Construction Limited limejengwa katika eneo la ekari 4.3 likiwa la ghorofa nne ambapo msingi wake ni wa ghorofa saba, ambapo ujenzi wake umezingatia mambo mbalimbali kuhimu ikiwemo usalama.

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR       

Previous Post

CCM YAANIKA MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA NDUGAI

Next Post

MASELE ACHUKUA FOMU YA U-SPIKA

admin

admin

Next Post
MASELE ACHUKUA FOMU YA U-SPIKA

MASELE ACHUKUA FOMU YA U-SPIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Instagram Youtube Twitter Facebook

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • autohenriquesevale.pt
  • best casino
  • Best online casino
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • Casino No Deposit Bonus
  • Casino UK
  • casino1
  • casino2
  • casino3
  • casino4
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • gambling platform
  • gambling platforms
  • Gry
  • gry hazardowe
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • mew casino
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • Nasi Partnerzy
  • new casino
  • niam.cl
  • non gamstop casinos
  • Nos partenaires
  • OM cc
  • Online Casino
  • Online Kasyno
  • Our Partners
  • Partners
  • Post
  • Pozyczki
  • Prestamos
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • sanodelucas.cl
  • SIASA
  • Slots
  • Sports
  • test
  • The best new online casino
  • The best online casino and sportsbook
  • UK Casino
  • Uncategorized
  • Unsere Partner
  • veterinariarepublica.cl
  • wildbeauty.cl
  • www.kuss.cl
  • Микрокредит
  • Наши Партнеры

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved