Sunday, July 5, 2026
[gtranslate]
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result

DK. MWINYI AWAASA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR

>>>Awataka waandishi wa habari kuandika habari zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi

admin by admin
February 14, 2022
in Habari Kitaifa
0
DK. MWINYI AWAASA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali kuendelea kuwa wabunifu katika kuandika habari na hasa zile zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya gazeti la Zanzibar Leo, zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Kiembesamaki, mjini Zanzibar.

“Kwa mnasaba huo, uongozi na wafanyakazi wa gazeti hili mnapaswa kufanyakazi zenu kwa weledi ili kuwafanya wananchi na wasomaji wote waweze kuliamini Gazeti letu kuwa ndicho chombo kinachotoa taarifa sahihi zilizoandikwa kwa umakini na zilizofanyiwa uchunguzi,” amesema Dk. Mwinyi.

Pia, Rais Dk. Mwinyi aliwahimiza viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Magazeti kwenda na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo imeongeza ushindani katika sekta ya habari kama ilivyo katika sekta nyingine.

Ameongeza kuwa miongoni mwa majukumu ya msingi ya gazeti la serikali la Zanzibar Leo ni kutoa taarifa sahihi, kwa wakati na zenye ubora, ili kukabiliana na ushindani uliopo hasa kutoka kwa magazeti ya kampuni binafsi.

Katika hotuba yake hiyo, Rais Dk. Mwinyi alivikumbusha   vyombo vya habari vya serikali kuwa mdomo wa serikali, kwa hivyo vinawajibu mkubwa wa kuisemea.

Amesema kuwa kutokana na kukua kwa tasnia ya habari na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani, wapo baadhi ya watu huitumia vibaya fursa ya uhuru wa habari kwa kupotosha, hivyo vyombo vya habari vya serikali vina jukumu la kuchukua hatua haraka za kuelezea usahihi wa taarifa kwa kutuma hoja, vielelezo na ufafanuzi wa jambo husika.

Rais Dk. Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwapongeza mawaziri wote kwa kutoa taarifa za kina juu ya utekelezaji wa majukumu ya wizara zao katika maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi na kutoa wito kuwa waendelee na utaratibu huo na usiwe katika kipindi cha sherehe pekee.

Aidha, aliwataka viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za serikali kuvitumia vyombo vya habari vya umma na vya binafsi kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali kwa umma, kubainisha changamoto pamoja na kueleza watakavyokabiliana na changamoto hizo.

Alieleza kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi na watendaji wa Shirika la Magazeti katika kuimarisha mazingira ya kufanyakazi pamoja na kuzifanyia kazi changamoto wanazo zikabili, huku akitumia fursa hiyo kutoa agizo kwa taasisi za serikali na sekta binafsi zinazodaiwa na shirika hilo kulipa madeni yao ili shirika liweze kuendesha shughuli zake.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa Serikali ya Mapinduzi ya awamu ya saba kwa kuwekeza fedha nyingi katika kuimarisha sekta ya habari hapa Zanzibar.

BAADHI ya Waalikwa na wafanyakazi wa Gazeti la Zanzibar leo wakiwa katika sherehe za kutimia miaka 20 ya gazeti hilo tokea kuanzishwa kwake zilizofanyika katika ukumbi Golden Tulip Hotel Kiembesamaki nje ya Jiji la Zanzibar.

Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, alitoa pongezi kwa Rais mstaafu wa awamu ya Sita  Dk. Amani Abeid Karume, kwa kuwa mwasisi wa gazeti hilo pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya saba Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuliendeleza na kuipa msukumo mkubwa sekta ya habari kupitia vyombo vya umma, likiwemo gazeti hilo.

Sambamba na hayo, Waziri Tabia alitoa pongezi kwa Rais Dk, Mwinyi kutoka kwa wadau mbalimbali kutokana na uamuzi wa kuzungumza na waandishi wa habari kila mwisho wa mwezi.

Pia, Waziri Tabia alitumia fursa hiyo kuwa pongeza wafadhili wote walio fadhili shughuli hiyo ambayo ili fana.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa gazeti la Zanzibar Leo, Ali Haji Mwadili akisoma risala ya kitaalamu ya Shirika la Magazeti ya Serikali alisema gazeti hilo lilianzishwa Januari 12  2022 na Rais mstaafu wa awamu wa sita Amani Abeid Karume likichukua nafasi ya gazeti la Nuru kwa lengo la kusambaza sera za serikali.

Aliongeza kuwa, kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Habari na uchumi wa buluu” alisema yenye lengo la kukumbusha umuhimu wa na mchango wa sekta ya habari katika maendeleo na mafanikio ya uchumi wa buluukwa kuwaelimisha na kuwahabarishawananchi.

Akieleza miongoni mwamafanikio mhariri mtendaji huyo alieleza kuwa ndani ya miaka 20 gazeti la Zanzibar Leo limezaa magazeti mengine manne ambayo ni Zanzibar Leo Jumaapili, Zasport, Zanzibar Mail pamoja na Zanzibar Leo wanawake, linalochapishwa kila mwisho wa mwezi, huku likipanua wigo wa usambazaji magazeti kwa mikoa 11 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Aidha,alieleza changamoto zinazolikabili gazeti hilo ikiwa ni pamoja na kupanda  kwa gharama za uchapishaji na usambazaji wa magazeti kutoka na kupanda kwa malighafi.

 Alisema wakati mwingine  wachapishaji hutaka faida kubwa ambapo kwa sasa asilimia 70 ya mapato ya shirika yanatumika katika uchapishaji. 

Alisema kutokana na maendeleo ya kimtandao na mabadiliko ya tasnia ya habari, magazeti duniani yanahitaji kuendana na matakwa hayo, ambapo kwa sasa shirika lina jipanga kuimarisha mitandao ya  kuendelea kuuza magazeti ya kwa njia ya mtandao.

Na MWANDISHI WETU

Previous Post

MTUHUMIWA WA MAUAJI NJOMBE ATIWA MBARONI

Next Post

RAIS SAMIA AWAALIKA WAWEKEZAJI WAFARANSA

admin

admin

Next Post
RAIS SAMIA AWAALIKA WAWEKEZAJI WAFARANSA

RAIS SAMIA AWAALIKA WAWEKEZAJI WAFARANSA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Instagram Youtube Twitter Facebook

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • autohenriquesevale.pt
  • best casino
  • Best online casino
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • Casino No Deposit Bonus
  • Casino UK
  • casino1
  • casino2
  • casino3
  • casino4
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • gambling platform
  • gambling platforms
  • Gry
  • gry hazardowe
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • mew casino
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • Nasi Partnerzy
  • new casino
  • niam.cl
  • non gamstop casinos
  • Nos partenaires
  • OM cc
  • Online Casino
  • Online Kasyno
  • Our Partners
  • Partners
  • Post
  • Pozyczki
  • Prestamos
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • sanodelucas.cl
  • SIASA
  • Slots
  • Sports
  • test
  • The best new online casino
  • The best online casino and sportsbook
  • UK Casino
  • Uncategorized
  • Unsere Partner
  • veterinariarepublica.cl
  • wildbeauty.cl
  • www.kuss.cl
  • Микрокредит
  • Наши Партнеры

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved