Katibu Mwenezi wa Itikadi wa CCM Paul Makonda amekabidhiwa ofisi na kuzungumza kuhusu majukumu yake mpya huku akisema atakuwa mwaminifu ili asimuangushe Mungu pamoja na Mwenyekiti wa Chama Rais Samia Hassan Suluhu.
“Nitafanya kazi kwa uaminifu nisimuabishe Mungu na M/Kiti wa Chama kwa kupeleka jina langu”Makonda.
Makonda amesema atajifunza kwa viongozi waliomtangulia kama Shaka, Sophia Mjema pamoja na Nape Nnauye ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake hayo mapya ndani ya siasa.






























