#JOTOLAUSPIKA: UCHUKUAJI wa Fomu za kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lina zidi kushika kasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Kada wa Chama hicho Wakili Andrew Kevela ni miongoni mwa makada waliochukua fomu hiyo.
Kada huyo amechukua fomu katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Jijini Dar es Salaam, Januari 14,2022 , ambapo ameeleza kuwa amejitathimini na kuona ana uwezo na Sifa za kuongoza mhimili huo.
Wakili Kevela amesema “nimeamua kuchukua fomu ya Uspika nina imani naweza kuwatumikia wananchi kuleta maendeleo.
Kupitia kauli ya Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu tarehe 7/1/2022 kwenye kufunga kongamano la matembezi ya UVCCM kule Zanzibar la Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Vijana tujitokeze kugombea nafasi mbalimbali za kitaifa na atatulinda na vijana tusitumike kuwabeba watu , kauli ya Rais Samia mimi imenihamasisha kuchukua fomu ya Uspika wa Bunge la Tanzania na kuamini nitashinda nafasi hio dhidi ya wagombea wote. amesema Wakili Kevela.
Na Abdurahmani Jummane





























