KITUO cha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) cha Kivukoni jijini Dar es Salaam, kinatarajiwa kupanuliwa
kwa lengo la kuboresha huduma kwa abiria wa mabasi hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma DART, William Gatambi, aliwaambia waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana kuwa, kituo hicho kitafungwa rasmi Oktoba 20, mwaka huu kupisha ujenzi wa upanuzi wake unaotarajiwa kuanza Oktoba 21, Mwaka huu.
Kwa msingi huo, Gatambi alifafanua kuwa vituo vya mabasi ya daladala yanayoegeshwa na kuwachukua abiria katika eneo hilo la kituo, watalazimika kuhama kwa muda na kutumia vituo vilivyoko jirani na Jengo la Wizara
ya Ardhi, Mtaa wa Ohio na benki ya NBC hadi hapo ujenzi huo utakapokamilika, huku akiwaomba radhi abiria,
wamiliki wa daladala na wadau kwa jumla kwa usumbufu utakaojitokeza katika kipindi hicho.






























