Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang’ katika wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amekabidhi misaada hiyo leo tarehe 22 Desemba, 22,2023 kwa Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mhe. Mndeme amesema WanaShinyanga wanaungana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kutokana na janga lililotokea Hanang lililosababishwa mvua kubwa iliyoambana na tope, mawe na miti hivyo kupelekea vifo, mali kupotea, mifugo kufa, mashamba kuharibika, nyumba kuharibika.
“Sisi wana Shinyanga tukiwa sehemu ya Watanzania tulipoguswa na janga hili tulipokea kwa masikitiko makubwa, baada ya kupokea taarifa hii ya kusikitisha, wanashinyanga kwa mapenzi mema wakaona nao wamuunge mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan lakini vile vile wawaunge mkono wananchi wengine kutoa pole kwa wananchi wa Hanang hivyo tumefika hapa katika mji huu wa Katesh kuwasilisha kwako mhe. DC pole zetu ili kuonesha mshimamano, umoja na kwamba tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu ambapo kwa wenzetu wa Hanang wanapitia”,amesema Mhe. Mndeme.
“Kwa niaba ya wananchi wa Shinyanga ambao wamejitolea kutoa pole zao kwa ndugu zao wa Hanang, naomba nikakibidhi mifuko 1000 ya saruji, mchele kilo 700, unga wa mahindi kilo 355, unga lishe kilo 250,juisi katoni 500, chumvi pakti 90,sukari kilo 25,sabuni katoni 13,mafuta ya kula lita 5, viatu pea 43, nguo balo 30 kati ya balo hizo 27 zina nguo za wanaume na tatu nguo mchanganyiko”, amesema






























