Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi cheti cha shukrani ya udhamini Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao ( e-GA) Ricco Boma, kwenye Mkutano Mkuu wa 7 wa Mashirika ya Utangazaji ya Umma Kusini mwa Afrika (SABA).
Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 10 hadi 12 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kisiwani Unguja ambapo e-GA ni miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo.





























