Sunday, November 16, 2025
27 °c
Dar es Salaam
25 ° Thu
25 ° Fri
25 ° Sat
25 ° Sun
25 ° Mon
English English Kiswahili Kiswahili
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • English English
  • Kiswahili Kiswahili

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result
Mwanzo Habari Kitaifa

SHAKA ATAJA MAFANIKIO LUKUKI MIAKA 45 YA CCM

admin by admin
February 5, 2022
in Habari Kitaifa
0 0
0
SHAKA: WAPIGANIA VYEO HAWAWEZI KUTUYUMBISHA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka

0
SHARES
129
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Shaka Hamdu Shaka, amesema katika kipindi cha miaka 45 tangu kuzaliwa kwa CCM, Chama kimekuwa kinara kwa kuchochea mageuzi ya demokrasia Afrika kwa kuendelea kupiga vita siasa chafu zenye mrengo wa ubaguzi.

Amesisitiza CCM itaendelea kuwa Chama sikivu, makini na kujali dhima ya majadiliano kwa njia za kiungwana kuliko kuandamwa na vitisho, kebehi, ubabe au kushurutishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Musoma, Mkoa wa Mara kuhusu mafanikio ya chama hicho kikongwe barani Afrika, ndani ya miaka 45 tangu kilipozaliwa baada ya kuungana vyama vya TANU na Afro-Shiraz Party (ASP), mwaka 1977, alisema kuwa,

CCM iko tayari kupokea maoni, ushauri na maafikiano yanayoheshimu njia za kiungwana na kistaarabu kwa maslahi mapana ya Taifa.

“Kazi kubwa ya utekelezaji wa  sera kwa miaka yote ya utawala wa  CCM madarakani ni kuhakikisha umoja  wa kitaifa,  unadumu na kubaki tukipinga  siasa chafu  za  ukabila, rangi, dini au  ukanda badala yake, sera zake zimekuwa zikihimiza umoja  na mshikamano, hali ambayo imelifanya Taifa letu kuwa lenye utulivu, upendo na ushirikiano,” alisema.

MAFANIKIO YA CCM MIAKA 45

Akizungumzia mafanikio ambayo CCM inajivunia tangu kuzaliwa kwake, Shaka alisema kwamba, katika kipindi hicho, Chama kimeendelea kuwaongoza Watanzania katika kulinda uhuru wa nchi yao na harakati za kujiletea maendeleo yao.

Alisema mafanikio ya dhahiri, yameonekana kupitia utekelezaji wa sera zake mbalimbali na kujijengea uhalali wa kuongoza nchi katika dunia ya sasa yenye mazingira yanayobadilika kila mara.

“Moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ni kudumu na kuimarika kwa muungano wetu. Katika kipindi cha miaka 45 iliyopita, muungano wetu umezidi kuimarika kutokana na juhudi za makusudi za chama chetu kuhakikisha muungano wetu unadumu milele.

“Tumefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ziliyojitokeza katika muungano wetu.

Aliongeza kuwa: “Tumeweza kufanya mambo kadhaa mapya ambayo yamefanya mambo yaende vizuri zaidi. Kitendo cha kuungana kwa TANU na ASP, ndiyo kilichozaa chombo kilichokuwa na nguvu na uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na changamoto za muungano wetu.”

Alibainisha kwa sasa, muungano umekuwa mfano bora wa kuigwa si barani Afrika pekee, isipokuwa duniani kote ambapo Watanzania wameudhihirishia Ulimwengu kuwa, dhamira ya kuungana ni imara na haitetereki.

“Tutaendelea kuimarisha muungano wetu kwa faida ya nchi yetu na watu wetu. Tunafanya hivyo kwa kutambua faida kubwa na nyingi zinazotokana na muungano wetu ambazo kila mmoja wetu anazitambua,” alisema.

 UMOJA WA KITAIFA

Shaka alieleza kuwa, mafanikio mengine ambayo chama kinajivunia ni kuimarisha umoja wa kitaifa kama ilivokuwa kwa vyama vya TANU na ASP, sera za CCM zimeendelea kulenga katika kuwaunganisha Watanzania na kujenga taifa moja imara lenye watu wamoja.

Alisema licha ya tofauti za kisiasa, rangi, dini au kabila, kila mmoja anajivunia na kuona faraja kuwa Mtanzania na kuendelea kuimarisha amani, utulivu na mshikamano, mambo ambayo baadhi ya mataifa ya Afrika na duniani ni bidhaa adimu.

 “Tumeweza kufanikiwa kubaki kuwa na taifa lenye umoja na utulivu, licha ya nchi yetu kupitia katika kipindi kigumu cha mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na kuingia katika mfumo wa vyama vingi na uchumi wa soko huria. Licha ya umoja wetu hata ukomavu wa kisiasa wa wananchi wetu, pia umeimarika.

“Watanzania ni watu wasioyumba wala kubabaishwa. Ni watu makini, wachambuzi na watambuzi mahiri.

“Haya ni mafanikio makubwa, ni jambo la kujivunia. Lakini ni sifa kubwa kwa chama chetu ambacho ndicho kiliongoza mageuzi hayo nchini.

“CCM itaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kudumisha na kuendeleza umoja, amani na utulivu wa taifa letu,” alifafanua.

 HUDUMA ZA JAMII

Kwa mujibu wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, taifa limepiga hatua hatua na kupata mafanikio mbalimbali katika nyanja za kiuchumi na kijamii.

“Pamoja na kuwa bado nchi yetu ni maskini, hali za watu wetu ni bora zaidi sasa kuliko ilivyokuwa mwaka 1977. Watu wengi wana kipato kikubwa, wanaishi katika nyumba bora zaidi, wanavaa vizuri na wanakula vizuri.

“Utoaji wa huduma za elimu, huduma za afya, maji, barabara, umeme zimeimarika kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Haya yote yanatokana na sera sahihi na mipango mizuri ya Chama Cha Mapinduzi.

MWALIMU WA DEMOKRASIA

Kuhusu demokrasia, alieleza kuwa, CCM imekuwa mwalimu wa Demokrasia nchini, mataifa jirani na kimeweza kusimamia na kuongoza nchi kufanya uchaguzi, wananchi kutumia mamlaka na haki zao za kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani na Utulivu.

Aidha, alisema CCM ndani ya miaka 45, imefanikiwa kusimamia muundo wa sera, mikakati na aina ya siasa inayohitajika katika nyakati za sasa, jambo lililosaidia kulinda na kusimamia usalama wa taifa na watu wake ili kudumisha amani, umoja na kujivunia uhuru wake.

Alisema kazi kubwa ya utekelezaji wa  sera kwa miaka yote ya utawala wa CCM madarakani ni kuhakikisha umoja  wa kitaifa unadumu na kubaki kupinga  siasa chafu za ukabila, rangi, dini au  ukanda badala yake, sera zake zimekuwa zikihimiza umoja  na mshikamano hali ambayo imelifanya taifa kuwa lenye utulivu, upendo na ushirikiano.

“Katika nyakati zote, kila mwananchi amekuwa mlinzi wa Taifa lake, askari wa mstari wa mbele anayehakikisha hatokei adui akayejivisha koti la kuwa kibaraka au wakala, badala yake mapambano yameelekezwa dhidi ya maadui ujinga, umasikini na maradhi,” alisisitiza.

USHIRIKIANO KISIASA

Shaka alisema kwa miaka yote 45, CCM imekuwa mstari  wa mbele kuendeleza na kudumisha ujirani mwema ili kujenga haiba ya maendeleo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kudumisha uhusiano mwema, kuendeleza ushirikiano na vyama vingine rafiki na vya kidugu duniani ikiwemo kanda ya Afrika Mashariki.

Alieleza CCM, imeendeleza mahusiano hayo ili kuhakikisha ujirani mwema unadumu, unaendelezwa kwa kuwaletea manufaa wananchi wa Tanzania na mataifa mengine.

Vilevile, alisema CCM katika kipindi cha miaka 45, imekuwa chachu ya kuanzishwa kwa kamati ya nchi tano zilizo mstari wa mbele kusini mwa Afrika, kipindi ambacho mataifa kadhaa yalikuwa bado hayajapata uhuru.

Kwa kushirikiana na vyama vingine vya ukombozi, CCM kimekuwa na mchango kwa mataifa hayo kushamirisha juhudi za ukombozi hadi mataifa hayo yalipopata uhuru na kujitawala yenyewe.

“Dhana ya mfumo  wa demokrasia ya vyama vingi ni kutanuka kwa wigo wa demokrasia shirikishi, ushindani wa sera kwa sera, ujenzi wa hoja kwa nguvu ya hoja. Kwa kipindi chote cha miaka 45 CCM kimeendelea kuwa Chama sikivu na makini kwa nyakati zote.

“Kinapenda na kujali dhima ya majadiliano kwa njia za kiungwana kuliko kuandamwa na vitisho, kebehi, ubabe au kushuritishwa. CCM kipo tayari wakati wote kupokea maoni, ushauri na rai hatimaye kufikia kwa maafikiano yanayoheshimu njia za kiungwana na kistaarabu kwa maslahi mapana ya taifa letu,” Shaka alieleza.

Alitoa wito kwa Watanzania kuendeleza umoja, mshikamno wa taifa na kuendelea kuvisihi na kuviomba vyama vyote vya siasa nchini kuendeleze umoja wa kitaifa, kuthamini na kukuza ustawi wa demokrasia iliopo nchini.

Alisema yapo mataifa mengi duniani hivi sasa yanatamani yafanane na Tanzania lakini kwa bahati mbaya haiwezekani baada ya baadhi ya wanasiasa wao kuvuruga amani yao.

Shaka alisema mafanikio hayo yamekuwa msukumo mkubwa wa ujenzi wa imani kwa wananchi wa Tanzania na imani hiyo itaendelea kulindwa na kuheshimiwa kwa utiifu.

“Kwa namna ya pekee Chama Cha Mapinduzi kinamshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyojipambanua tangu alipochukua hatamu ya uongozi wa kuliongoza taifa kwani ameonyesha uwezo, juhudi na jinsi alivyodhamiria kukabiliana dhidi ya changamoto mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa katika kusukuma maendeleo endelevu ya nchi yetu,” Shaka alieleza.

NA MUSSA YUSUPH, MUSOMA

admin

admin

Stay Connected test

  • 139 Follower
  • 205k Subscriber
  • 23.9k Follower
  • 99 Subscriber
  • Trending
  • Comments
  • Latest
MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

MADAKTARI WAELEZEA JINSI YA KUZUIA MIMBA ISIHARIBIKE

July 9, 2021
BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

BREAKING NEWS: RATIBA LIGI KUU NBC MSIMU WA 2023/2024 HII HAPA

August 7, 2023
TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

TABWA YAMSIFU SAMIA KUWAPA FURSA WANAWAKE

July 9, 2021
BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

BEI MPYA YA MBAAZI, KUNDE YAWAPANDISHA MZUKA WAKULIMA

August 9, 2021
NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

NDUGU MATATANI KUMSHAMBULIA, KUMJERUHI MWENZAO KISA NG’OMBE

0
WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

WAHANDISI WA HALMASHAURI WAMEKUA WAKIIKOSEA SERIKALI KWAKUTOA TAARIFA ZA UONGO

0

OFISA ELIMU, MHANDISI, MKUU WA SHULE WAKALIA ‘KUTI KAVU’

0
STENDI YA ZAMANI UBUNGO  KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

STENDI YA ZAMANI UBUNGO KUJENGWA DEPO MABASI MWENDOKASI

0

Exploring Herbal Viagra Alternatives: Natural Solutions for Men’s Health

May 23, 2025
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 12, 2024

November 12, 2024
YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

YALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 11, 2024

November 11, 2024

Recent News

Instagram Youtube Twitter Facebook

We are a diverse team of experts, innovative thinkers, creative designers, writers, innovators, strategists, pyschologists, comunictaors and web developers. UMG is extremely passionate about growing clients’ businesses, helping them achieve their goals and making a difference by raising the creative and communications industry standards in Tanzania.

Follow Us

Browse by Category

  • 231
  • Afya Makala
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • RIWAYA
  • SIASA
  • Sports
  • Uncategorized

Recent News

Exploring Herbal Viagra Alternatives: Natural Solutions for Men’s Health

May 23, 2025
TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

TALIYOJIRI KATIKA GAZETI LA UELEKEO LEO NOVEMBA 20, 2024

November 20, 2024

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In