SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewaomba radhi watanzania juu ya taarifa za uchochezi dhidi yake kuhusu kupinga mkopo wa serikali.
Ameyasema hayo leo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema anaungana na wabunge wengine wote katika kupongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kupambania maendeleo ya watanzania kwa kuwarahisishia huduma mbalimbali za kijamii.
Amesisitiza kuwa kusambaa kwa taarifa hizo zimeleta sintofahamu kwa watanzania jambo ambalo limemletea kashifa kwakuto pongeza dhamira ya serikali juu ya Mkopo wa Trilion 1.3 uliotolewa na Bank ya Dunia juu ya maendeleo ya Uviko 19.
“Mimi kama mbunge nimekuwa shahidi mkubwa sana juu ya maendeleo ya ujenzi wa shule zetu za kata kutokana na mkopo tulioupata kwa kweli madarasa ni yakisasa kabisa hayajawai tokea hapa nchini”. Aliendelea
“Haijawai tokea serikali inawekeza fedha nyingi kiasi hiki kwaajili ya maendeleo ya Taifa letu na kwakweli tunampongeza sana Rais Samia Suluhu Hassani kwa hiki alichokifanya”. Alisema Spika Job.
Aidha Spika Ndugai amewataka wabunge kurejea jijini Dodoma kwa ajili ya kukutana na kamati zao ili kujiandaa na vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza mwenzi wa Pili mwaka huu.
Na.Benedict Mwasapi





























