Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete, Ndg. Willam Makufwe, ameziomba taasisi mbalimbali, wilayani humo, kuhakikisha kuwa zinapambana na ukatili kwa watoto wadogo ili kuwa na kizazi kijacho chenye weledi na uelewa.
Ndg. Makufwe, amesema hayo Novemba 29, 2023, kwenye kikao cha Uzinduzi wa Jukwaa la Wadau wa Ustawi wa Mtoto, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete kuwa kila mtu awe mlinzi wa mtoto, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili katika jamii inayowazunguka.
“kila mtu akawe mlinzi wa watoto, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili, pamoja na kuwasaidia wale ambao wanaishi kwenye mazingira magumu kwakuwa wanauhitaji kama watoto wengine” Alisema Makufwe.





























