Sunday, July 5, 2026
[gtranslate]
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result

UHAMISHAJI WAMACHINGA WAIIBUA CCM

Nov. 1, 2021>>Serikali ya Mkoa Dar ilitangaza kuanza marufuku bodaboda kuingia katikati ya jiji

admin by admin
November 1, 2021
in Habari Kitaifa
0
CCM YATIA MKONO TRILIONI 1.3/- ZA IMF

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka

Msimamo wa Chama ni kuwalinda ili wasiyumbe kiuchumi, aidha ni marufuku bodaboda, bajaji kuzuiwa kuingia katikati ya jiji…wenyewe wafurahia wasema chama kimebeba kilio chao.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo kuhusu operesheni ya kuwahamisha wamachinga ambapo imewaonya wale wanaofanya kazi hiyo bila kuzingatia maelekezo na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kimesema maagizo na maelekezo ya Rais Samia kuhusu wamachinga, ni kuhamishiwa katika maeneo yaliyo bora zaidi yakiwa na miundombinu rafiki ili waendeshe shughuli zao kwa ufanisi.

Chama kimesema kuanzia sasa hakitakuwa tayari kuona kundi hilo la wananchi waliojiajiri likinyanyaswa na kwamba sehemu yoyote kutakapobainika kufanya hivyo chama kitachukua hatua ikiwemo kuzishauri mamlaka za uteuzi dhidi ya mtumishi au kiongozi aliyehusika.

Pia, kimetoa maelekezo mbalimbali ikiwemo kutaka kusitishwa kwa zuio dhidi ya bodaboda na bajaji zisizokuwa za watu wenye ulemavu kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Hayo yalielezwa  na Katibu wa Halmashauri Kuuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chama kuhusu hatua zinazochukuliwa na baadhi ya viongozi katika maeneo mbalimbali nchini.

“Baada ya kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa uamuzi huo wa kisera uliofanywa na serikali, Chama kinaelekeza kwamba, kitendo cha kuwahamisha Machinga bila kuwaandalia maeneo mbadala ambayo yameboreshwa kwa kuwekewa miundombinu kwa ajili ya shughuli zao, ni marufuku na hakikubaliki,” alisema.

Shaka alisema CCM, ndiyo iliyopewa dhamana ya kuongoza nchi na kuunda Serikali baada ya kunadi ahadi na sera zake kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020 -2025, ambayo kimsingi ndio mkataba kati yake na wananchi.

Alisema moja ya maeneo yaliyopewa msisitizo mkubwa katika ahadi na sera za CCM kupitia Ilani ya Uchaguzi, ni kuongeza ajira, kurasimisha na kuiwekea mazingira rafiki na wezeshi sekta isiyo rasmi.

“Hayo yameelezwa kwenye Ilani yetu ya uchaguzi Ibara za 8(f), 9(F), 32(C), (q) na 122(m). Maelekezo haya ya Ilani yamezingatia ukweli kwamba sekta isiyo rasmi ni sekta muhimu kwa mustakabali wa ustawi wa uchumi hapa nchini, yenye nafasi kubwa ya kutoa ajira, kustawisha maisha ya wananchi na kutokomeza umaskini.

“Aidha, maeneo mengi ya miji nchini ni kitovu cha biashara ambapo wananchi walio wengi wamejiajiri katika sekta isiyo rasmi, wengi wao wakiwa ni vijana na wanawake makundi ambayo ni sehemu kubwa ya wakazi hapa nchini,” alisema.

Shaka alisema huko nyuma iliaminika kuwa, wananchi wengi waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi walionekana ni wenye kiwango kidogo cha elimu, lakini sasa wahitimu wengi wa vyuo vya elimu ya juu nao wamejiajiri katka sekta hiyo.

“Hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii, CCM lazima ibebe wajibu wa msingi wa kulinda maslahi ya wote waliojiajiri hapa,” alisema.

Alisema maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa viongozi na watendaji wa serikali kuhusu kuwapanga upya  wamachinga na mamalishe, ni kutumia njia bora bila nguvu ili waendelee kufanya shughuli zao kwa utulivu.

“Mheshimiwa Rais Samia alisisitiza upangaji huo uambatane na wafanyabiashara hao kupewa maeneo ya kufanyia biashara zao Pamoja na kuwekewa miundombinu mizuri. CCM inawapongeza wafanyabiashara wadogo kwa mapokeo chanya kuhusu agizo la Rais Samia.

Kwa mujibu wa Shaka, Chama kimekuwa kikifuatilia kwa karibu utekelezaji wa maelekezo ya kuhusu wamachinga na kubaini dosari nyingi ikiwemo kundi hilo kutoshirikishwa kikamilifu.

Aliitaja dosari nyingine ni mapendekezo ya wamachinga kutokusikilizwa, maeneo wanyotakiwa kuhamia kutoainishwa, kuhamishwa kimakosa kwa baadhi ya maeneo, matumizi ya nguvu kubwa kiasi cha kuharibu mali, mitaji pamoja na muda uliowekwa kuwa mdogo sana.

APIGA MARUFUKU ZUIO LA BODABODA MJINI

Akizungumzia kuzuiwa kwa waendeshaji wa bodaboda na Bajaji kuingia katikati ya jiji, alisema maelekezo ya CCM kuhusu jambo hilo ambalo utekelezaji wake ulipaswa kuanza leo ni kusitishwa kwa jambo hilo.

“Marufuku ya waendesha/watumiaji wa bodaboda na bajaji kutofika au kutofanya shughuli zao katikati ya jiji la Dar es Salaam si mwafaka, imetolewa bila kuzingatia taratibu za msingi zinazopaswa kutumika kufanya uamuzi unaogusa maslahi ya wananchi, kama huo, hivyo Chama kimeagiza isitishwe mara moja.

Mbali na hilo, Shaka alisema mamlaka za serikali Dar es Salaam, zinazohusisha viongozi, watendaji wa umma, vyombo vya dola na mamlaka zingine zenye majukumu ya kusimamia usafiri na usafirishaji maeneo mbalimbali ya jiji hilo, chini ya Mkuu wa Mkoa (Amos Makala), kwa kuwashirikisha wadau wengine, wakutane haraka iwezekanavyo kuangalia iwapo kuna changamoto zimejitokeza ili zijadiliwe kupata ufumbuzi wa muda mfupi wa kati na muda mrefu, bila kuathiri wala kubugudhi ustawi wa shughuli za makundi ya watu yanayohusika.

“Chama kinasisitiza kuwa, kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, kitafuatilia mrejesho na utekelezaji wake,” alisema.

Alisena kupitia taarifa hiyo, Chama kinaelekeza kuwa amri au maagizo yoyote, yanayogusa maslahi na agenda za wananchi ambazo CCM iliahidi kuzisimamia kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025, yanapaswa kutolewa kwa umma na mamlaka za kamati za ulinzi na usalama katika mikoa na wilaya baada ya suala husika kujadiliwa na kufanyiwa uamuzi katika vikao.

“…Pia ni muhimu kufanya mawasiliano na mashauriano na wadau kwenye nyanja inayohusika,” alisema.

ONYO

Shaka alisema Chama kinaonya kuhusu utaratibu unaoanza kuibuka wa baadhi ya watu kujichukulia mamlaka ya kutoa kauli au maagizo ambayo hayatokani na uamuzi wa vikao ambavyo vimewekewa utaratibu wa kisheria, kulingana na uendeshaji na utendaji kazi wa mamlaka za kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya, hali ambayo inaibua sintofahamu na hata chuki katika jamii.

“Chama kinawakumbusha viongozi na watendaji wa serikali kuwa uamuzi wa serikali uliotangazwa na Rais Samia wa kuwapanga na kuwahamisha wamachinga, uliwekewa msisitizo wa kuhakikisha maeneo wanayopangwa au kuhamishiwa yanakuwa yameandaliwa na kuwekewa miundombinu rafiki, kwa ajili ya shughuli za waachinga na wateja wao kuendelea bila kukwamisha fursa za kujitafutia kipato na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.

Alisema Chama kinafuatilia kwa ukaribu operesheni hiyo katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

“Katu hakitakubali wala kuachia liendeshwe kinyume na ilivyoagizwa na maamuzi hayo ya serikali. CCM haitasita kuanzisha hoja au agenda ya kuhakikisha wote wanaokiuka maelekezo ya namna ya kuwapanga Machinga, wanaondolewa katika nafasi zao, kuliko kuwaacha wakizalisha athari hasi katika jamii,” alisema.

Alizitaka kamati za siasa na wilaya na mikoa kufuatilia kwa karibu jambo hilo na kusema popote ambapo utekelezaji wake utakwenda kinyume na maelekezo ya Rais Samia basi nazo zitawajibika.

BODABODA, WAMACHINGA KICHEKO

Shirikisho la Vyama vya Waendesha Bodaboda Dar es Salaam limepongeza hatua hiyo ya CCM kuingilia kati usitishaji wa pikipiki kuingia katikati ya jiji.

Mwenyekiti wa  Shirikisho hilo, Said Chenja, alisema walisikitika kwa hatua iliyotangazwa awali na uongozi wa mkoa huo kusitisha pikipiki kuingia  mjini.

“Tulisikitika sana. Serikali haiwezi kutuajiri wote.  Tunaishukuru CCM kupitia kwa msemaji wake Shaka  kwa msimamo huo,” alisema.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Machinga Tanzania, Steven Lusinde, alipongeza hatua ya CCM kuingilia kati suala hilo kwani tatizo lililojitokeza siyo wamachinga kutotii maelekezo bali ni baadhi ya maeneo wanayopelekwa  kutokuwa rafiki kwa biashara zao.

“Tunakishukuru kwa ujumla wake  Chama, kwamba machinga hawana shida na ndiyo maana katika majiji yote waliondoka wenyewe, changamoto inayo kuja ni ya viongozi kulazimisha  waondoke wakati  hawana pa kuwapeleka katika baadhi ya maeneo. ieIeweke kuwa mmachinga  mazingira yake ya  biashara ni yawapita njia. Sasa mtu unampeleka  Kigilagila atauza nini?”alisema Lusinde.

AGIZO LA RAIS SAMIA

Akilihutubia taifa baada ya kuwaapisha mawaziri wanne na mwanasheria mkuu wa serikali, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, wiki kadhaa zilizopita, Rais Samia aliwaagiza wakuu wa mikoa kote nchini, kuliangalia upya suala la wamachinga na kuwapanga upya katika maeneo, wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la wamachinga.

Pia Rais Samia alitahadharisha kuwa, agizo hilo halina maana utekelezaji wake uhusishe matumizi ya nguvu, mabavu yatakayoleta hali ya kutoelewana baina ya wamachinga, serikali na wafanyabiashara wenye maduka.

“Wito wangu kupitia jukwaa hili, kwa wakuu wa mikoa kuchukua hatua za kuwapanga vyema, na ninaposema kuchukua hatua kuwapanga vyema sitaki kuona yale ninayoyaona kwenye Tv, ngumi, kupigana, kufukuzana, vitu kumwagwa aaah aah,” alisema.

Katika hotuba hiyo, Rais Samia alisema, awali serikali ilitoa fursa kubwa kwa wamachinga kufanya biashara zao kama moja ya njia za kujipatia riziki ya kila siku, hivyo kuipunguzia mzigo serikali.

Na MWANDISHI WETU

Previous Post

BILIONI 10 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI SIMIYU

Next Post

JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI KUTOCHELEWESHA UTOAJI  HAKI

admin

admin

Next Post
JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI KUTOCHELEWESHA UTOAJI  HAKI

JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI KUTOCHELEWESHA UTOAJI  HAKI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Instagram Youtube Twitter Facebook

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • autohenriquesevale.pt
  • best casino
  • Best online casino
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • Casino No Deposit Bonus
  • Casino UK
  • casino1
  • casino2
  • casino3
  • casino4
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • gambling platform
  • gambling platforms
  • Gry
  • gry hazardowe
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • mew casino
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • Nasi Partnerzy
  • new casino
  • niam.cl
  • non gamstop casinos
  • Nos partenaires
  • OM cc
  • Online Casino
  • Online Kasyno
  • Our Partners
  • Partners
  • Post
  • Pozyczki
  • Prestamos
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • sanodelucas.cl
  • SIASA
  • Slots
  • Sports
  • test
  • The best new online casino
  • The best online casino and sportsbook
  • UK Casino
  • Uncategorized
  • Unsere Partner
  • veterinariarepublica.cl
  • wildbeauty.cl
  • www.kuss.cl
  • Микрокредит
  • Наши Партнеры

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved