WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku akiwataka watumishi wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuhakikisha wagonjwa wanaokwenda wanapata huduma.
Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) amefanya ziara ya kutembelea kwenye hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alizungumza na timu ya hospitali hiyo (HMT) ambapo aliwataka madaktari na wauguzi kuhakikisha wanatoa maelezo sahihi ya wagonjwa wanaolazwa na ndugu.
Amesema hatua hiyo itawaepusha kuwaondolea wagonjwa sintofahamu hususani wanapokuwa wakiulizwa na aina ya ugonjwa anapouluzwa na ndugu zake .
Akiwa kwenye mazungumzo hayo aliwataka watumishi wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa waledi mkubwa hususani katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupata huduma za matibabu.
Hata hivyo amewapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwatiaa moyo huku akiwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.




















