Imebainishwa kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwajengea uwezo watunga sera hasa makatibu wakuu
na Wabunge kuhusu athari za matumizi mabaya ya ardhikatika maeneo ya vyanzo vya maji, Mito na kandokando ya Bahari ili kuwa nauelewa wa pamoja wa athari hizo na mna ya kukabiliana nazo kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo
Wito huo umetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua mafunzo ya siku saba kwa viongoziwaandamizi wanaosimamia masuala ya maji na mazingira kutoka nchi 10 za Afrika zilizo kwenye ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi yanayofanyika Jijini
Mbeya kupitia mradi wa Utafiti wa Usimamizi Endelevu wa Madakio ya Maji Kupitia Tathmini ya Kuimarisha Mtiririko wa Maji kwa Mazingira na Utekelezaji
wake katika Kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi na Athari za Shughuli za Kibinadamu Tanzania (EFLOWS).
“Pamoja na kazi kubwa ambayo nyinyi kama wataalamu mnaifanya mwisho wasiku mtaandaa tarifa nzuri na kuwapelekea watunga sera ili waifanyie kazi, Lakinibila wao kuelewa vizuri kwa kina mnayoandika baada ya kufanya tafiti mtajikutataarifa zenu mnazowaandikia hazifanyiwi kazi kama mnavyotegemea hivyo kunaumuhimu mkubwa sana wa kujengeana uwezo nyinyi lakini pia kuwajengeauwezo pia watunga sera maana ndio mnaowategemea katika kutelekeza yalemnayowaplekea” Alifafanua Prof. Chibunda.
Amesema kuwa kuna tafiti nyingi sana zinafanyika kwenye nchi mbalimbali nahata Tanzania ambazo zinalenga kutatua changamoto fulani lakini matokeo yakehayaonekani moja kwa moja kwa jamii na Taifa kwakuwa wale wanaotegemewakuchukua matokeo hayo na kuyatumia pengine hawayatumii kwakuwa hawanauelewa wa kina na wakutosha kuhusu yale ambayo tafiti zimebainisha.
Amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na Watafiti kutoka SUA kwa kushirikiana naBaraza la Taifa la Hifadhi ya mazingira NEMC katika utekelezaji wa Mradi waTathimini ya maji kwa mazingira ambao matokeo yake mazuri ndio yamepekekeaWataalamu hao kutoka nchi zote washiriki kuleta wataalamu wao kuja kujifunzana kupanga mikakati ya pamoja na kukabiliana na changamoto hizo zakimazingira.
Awali akieleza malengo ya mafunzo hayo Mtafiti Mkuu wa Mradi wa EFLOWSambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za Uzamili, Utafiti, Uhauwilishaji wateknolojia na Ushauri wa Kitaalamu kutoka SUA Prof. Japhet Kashaigili amesema
utaalamu huo wa Tathimini ya maji kwa mazingira ambao umejengwa kupitiamradi huo imeonekana ni muhimu sasa kuweza kuusambaza kwa wataalamukwenye nchi hizo ili kuwa na uelewa wa pamoja wa kukabiliana na changamotohizo za kimazingira.
utaalamu huo wa Tathimini ya maji kwa mazingira ambao umejengwa kupitiamradi huo imeonekana ni muhimu sasa kuweza kuusambaza kwa wataalamukwenye nchi hizo ili kuwa na uelewa wa pamoja wa kukabiliana na changamotohizo za kimazingira.
“Mradi wa EFLOWS ambao tumeufanya kwa miaka miwili Wilayani MbaraliMkoani Mbeya na Wanging’ombe Mkoani Njombe ulikuwa mradi wa mfanokuangali mtiririko wa maji na hali ya mto Mbarali matokeo yake yalilenga kupataelimu ambayo itatumiwa na nchi zingine 10 za afrika, hivyo baada ya kukamilikakwake sasa tumewaita wataalamu waandamizi kutoka nchi hizo kuja Tanzaniatujifunze na kubadilishana uzoefu kutokana na matokeo tuliyoyapata na kishakuja na maazimio ya pamoja ya namna ya kulinda ukanda wa magharibi mwaBahari ya Hindi kupitia mito na vyanzo vyake” alifafanua Prof. Kashaigili.
Aidha amesema kuwa changamoto nyingi za kimazingira zinazoonekana sasa duniani ni matokeo ya shughuli za kibindamu ambazo zinagusa sekta mbalimbalihivyo kutatua changamoto hizo ni lazima kuwe na jitihada za pamoja za kila mdaukwenye sekta hizo na ndio maana wanawajengea uwezo kutambua na kuwekamikakati ya pamoja ili kupata matokeo makubwa kwa wakati.
Aidha amesema kuwa changamoto nyingi za kimazingira zinazoonekana sasa duniani ni matokeo ya shughuli za kibindamu ambazo zinagusa sekta mbalimbalihivyo kutatua changamoto hizo ni lazima kuwe na jitihada za pamoja za kila mdaukwenye sekta hizo na ndio maana wanawajengea uwezo kutambua na kuwekamikakati ya pamoja ili kupata matokeo makubwa kwa wakati.
Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mkuu kutoka ofisi ya Makamu wa RaisBwana Wankyo Mnono amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa nchi zotewanachama kwakuwa ulinzi wa Ikolojia ya Bahari ni muhimu kwa ustawi waviumbe na maisha ya watu maisha yao yanategemea rasilimali zinazopatikanabaharini.
“Tunatumia samaki na viumbe maji vingine kutoka Baharini na kwenye mito hivyoswala la ulinzi wa ikolojia ya maisha ya samaki na viumbe vingine ni muhimu kwakuweka mipango na mikakati mizuri ya kuvilinda ili viendelee kutoa mchango kwajamii na taifa vizazi hadi vizazi lakini hilo litawezekana kama kutakuwa naushirikiano kwa nchi zote zilizo ukanda wa magharibi mwa bahari ya Hindi”alieleza Bwana Wankyo.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa kulinda Bahari na ikolojia yake Serikali yaTanzania inatarajia kutekeleza mradi mdogo wa utafiti utakaoangalia hali namadhara ya matumizi ya mifuko na vifungashio vingine vya plastiki ili kupatataarifa ambazo zitasaidia nchi kufanya maamuzi muhimu ya namna ya kukabilianana athari zinazotokana na matumzi ya plastiki kwenye bahari na nchi kavu.
Akitoa salamu kutoka Sekretarieti ya Azimio la Nairobi ambao ndio wafadhili wamradi huo Bwana Sammy Weru ameishukuru Serikali ya Tanzania na Chuo kikuucha Sokoine cha Kilimo kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ya Kikandaambayo yana mchango mkubwa katika kulinda na kusimamia ukanda huo wabahari ya Hindi.
“Tunajisikia furaha kufanya kazi na SUA katika kutelekeza miradi mbalimbaliyenye tija kubwa kwa nchi zetu, na ninaamini kuwa kupitia mafunzo hayatutatengeneza miongozo ya namna kusimamia masuala ya tathimini ya maji kwamazingira lakini bila kusahau kuzingatia dhana ya “kutoka Chanzo hadi baharini”katika kuhakikisha usalama wa viumbe maji na ikolojia zao” alieleza Bwana Weru.
Mradi wa Utafiti wa Usimamizi Endelevu wa Madakio ya Maji Kupitia Tathmini ya Kuimarisha Mtiririko wa Maji kwa Mazingira na Utekelezaji wake katika Kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi na Athari za Shughuli za Kibinadamu.
Tanzania (EFLOWS) unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la hifadhi ya mazingira NEMC na wad au wengine kwa ufadhili wa Sekretarieti ya Azimio la Nairobi.