HUKUMU ya kesi ya Jinai ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkali aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya(34) na wenzake wawili imeahirishwa hadi Oktoba 15 mwaka huu kutokana maandalizi ya hukumu kutokamilika.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Amalia Mushi, amedai mahakamani hapo kuwa maamuzi ya maandalizi ya hukumu hayajakamilika kuandaliwa.
Waashtakiwa wengine katika kesi hiyo namba 105 ni pamoja na Silyvester Nyegu (26) na Daniel Mbura (38).





























