DARASA la uokaji wa Keki wahitimishwa Kwa chakula cha jioni na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania katika ukumbi wa Kilimanjaro jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wahabari Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mehmet Gilly, amempongeza Muandaaji wa Darasa hilo, Zena Sharif kwa kuiona fursa ya Waokaji hapa nchini na nje ya nchi, kuongeza ujuzi katika biashara zao hususan upishi wa keki zenye ufundi na stadi wa Hali ya juu.
Mafunzo hayo yatawanufaisha wahitimu pamoja na wafanyabiashara wote hususan Waokaji wa Keki kwani kupitia biashara hiyo ni sehemu ya watu kujipatia vipato vyao kama biashara zingine.
Hata hivyo Balozi amewasihi wahitimu hao kuendeleza ujuzi huo waliopata kwa Waokaji wengine Ili kukuza na kuboresha Biashara ya Keki Kimataifa.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Kimataifa chifu Tuba amesema, katika nchi alizotoa Mafunzo Tanzania imekua nchi ya kwanza kuwa na wanafunzi waliojifunza Kwa haraka zaidi japo kumekuwa na baadhi ya changamoto ya Lugha ya Mawasiliano kuwa ngumu kutokana na yeye kujua lugha ya kingereza kwa uchache.
Mmoja wa wanafunzi ambao walioshiriki darasa Hilo ambaye pia ni Muigizaji wa ‘Bongomovie’ Eshe Buheti, amesema kutengeneza keki zenye maumbo haikua kitu rahisi kwani kuna ufundi ambao kama mpishi unahitajika kufahamu vitu vingi Ili kuwezesha kukamilsha maumbo hayo.
“Nilikata Tamaa japo naweza kupika keki lakini kuna baadhi ya vitu vya utofauti wateja wanahitaji kama keki zenye mfanano wa maumbo hivyo kama mpishi unalazimika kufahamu Ili kuboresha Biashara yako na kwakupitia darasa hili nimeweza kufuzu na najiandaa kwa wateja, ” Amesema.
Na AMINA KASHEBA





























