Sunday, July 5, 2026
[gtranslate]
UMG
  • Mwanzo
  • UMG
  • Siasa
    • All
    • Business
    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    SHIRIKA LA OMUKA HUB NA NDI WAANDAA MAJADILIANO YA JUKWAA LA WANAWAKE KATIKA SIASA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    WAZIRI JAFO ATETA NA WAKUU WA MIKOA

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU MWENYEKITI UVCCM AWAJIA JUU WANAOWACHAFUA VIONGOZI

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    MAKAMU WA RAIS DK. PHILIP MPANGO AKIONDOKA NCHINI ANGOLA

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    FORBES YAMTAJA TENA RAIS SAMIA.. “NI MIONGONI MWA WANAWAKE 100 WENYE UWEZO MKUBWA DUNIANI”

    Trending Tags

    • Trump Inauguration
    • United Stated
    • White House
    • Market Stories
    • Election Results
  • Biashara
    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTHIBITISHA UBORA WA BIDHAA NJOMBE

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    SHERIA YA LOCAL CONTENT INAVYONUFAISHA WAWEKEZAJI WAZAWA GGML

    Trending Tags

    • Nintendo Switch
    • CES 2017
    • Playstation 4 Pro
    • Mark Zuckerberg
  • Burudani
    • All
    • Sports
    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    YANGA YAMNYATIA ABIALA KUTOKA CONGO DR

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

    SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0

  • Michezo
    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    SERIKALI YAAHIDI KUWAPELEKA MASHABIKI WA YANGA AFRIKA KUSINI

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    YANGA SC YAACHANA NA MOLOKO

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    TFF YAUFUNGIA UWANJA WA UHURU

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    BENCHIKHA; MCHEZO WA KESHO UTACHORA RAMANI KUELEKEA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA WYDAD CASABLANCA

    Trending Tags

    • MotoGP 2017
    • eSports
    • Fashion Week
  • MAGAZETI
    • UELEKEO
  • UMG DIGITAL
  • UELEKEO DIGITAL
    • Instagram
    • Facebook
    • Twitter
    • Youtube

No Result
View All Result
UMG
No Result
View All Result

UCHUMI TANZANIA WAZIDI KUIMARIKA

Asilimia 4.7>>>Mwenendo wa ukuaji uchumi wa ndani Tanzania Bara nusu ya kwanza

admin by admin
November 16, 2021
in Habari Kitaifa
0
UCHUMI TANZANIA WAZIDI KUIMARIKA

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, amesema mwenendo wa uchumi wa ndani Tanzania Bara, umeendelea kuimarika hadi kufikia asilimia 4.7 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2021.

Kadhalika, uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia 6.5 katika robo ya pili ya mwaka 2020, ikilinganishwa na ukuaji hasi wa asilimia 1.4 katika robo ya pili ya mwaka 2020.

Profesa Luoga amebainisha hayo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ambapo amesema matokeo hayo yamebainishwa na Kamati ya Sera ya Fedha ya BoT, iliyokutana mwanzoni mwa wiki hii.

Katika taarifa hiyo, Gavana alisema kamati imebaini kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia imekuwa chini kidogo ya matarajio ya awali yaliyowekwa kidunia.

Alieleza hali hiyo imetokana na kuibuka upya kwa janga la Uviko-19 katika baadhi ya nchi na kupanda kwa bei za nishati duniani.

“Hata hivyo, ukuaji huu wa uchumi wa dunia unatarajia kuchangia kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Tanzania,” alieleza Gavana katika taarifa yake.

Alisema kamati ya sera ya fedha imeridhishwa na utekelezaji wa sera ya fedha kwa kipindi cha Septemba na Oktoba, mwaka huu, ambao uliwezesha kuendelea kuwepo ukwasi wa kutosha katika sekta ya benki.

Profesa Luoga alisema hali hiyo ilichangia mwenendo wa riba katika soko la fedha kuendelea kuwa tulivu na katika viwango vya chini.

Gavana huyo alieleza ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, umeimarika kufikia asilimia 4.6 kwa mwaka ulioishia Septemba 2021, kutoka asilimia 3.2, iliyokuwepo Agosti.

Amesema kamati hiyo pia imejiridhisha kasi ya ukuaji wa mikopo katika sekta binafsi inatarajiwa kuendelea kuimarika kwa sababu ya vichocheo mbalimbali.

Mojawapo amesema ni kuimarika uchumi wa dunia na hatua za kisera zilizochukuliwa na Benki Kuu ili kuchochea upatikanaji wa mikopo kwa riba nafuu.

FEDHA ZA KIGENI

Kwa mujibu wa Gavana Luoga, akiba ya fedha za kigeni nchini, imeendelea kuwa ya kuridhisha na kufikia Dola za Marekani bilioni 6.7 hadi kufikia Oktoba, mwaka huu.

Alisema kiasi hicho kinatosheleza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi saba sawa na lengo la nchi na makubaliano ya jumuiya za kikanda.

MFUMUKO WA BEI

Katika taarifa yake, Gavana alisema mifumuko ya bei duniani, imekuwa ikipanda kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na kupanda bei za nishati.

Hata hivyo, alisema Benki Kuu nyingi duniani zinaona ongezeko hilo kuwa la mpito, hivyo kuendelea na sera ya fedha yenye kuongeza ukwasi katika uchumi.

Alisema mfumuko wa bei uliendelea kubaki ndani ya lengo la asilimia kati ya 3 hadi 5, sanjari na makubaliano ya kikanda kwa nchi za EAC na SADC.

“Mfumuko wa bei unatarajiwa kusalia sambamba na lengo, licha ya kuongezeka kidogo tangu mwezi Juni 2021,” alieleza Gavana Luoga.

Pia aliongeza kuwa: “Kamati inaamini kwamba kuongezeka uzalishaji wa mafuta duniani kutapunguza kupanda kwa bei ya nishati.”

Alisema pamoja na hayo, kamati inasisitiza umuhimu wa kuendelea kwa upatikanaji wa chakula cha kutosha nchini na uimara wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni kunakotarajia kupunguza athari ya kupanda kwa bei ya mafuta kwenye mfumuko wa bei.

UKUSANYAJI MAPATO

Gavana Luoga alisema ukusanyaji wa mapato ulikuwa wa kuridhisha, huku mapato ya kodi yakiwa zaidi ya asilimia 90 ya lengo.

Alisema mfumuko wa bei uliendelea kuwa chini ya lengo la asilimia 5, huku ukusanyaji wa mapato ukiwa sawa na asilimia 73.6 ya lengo.

Kwa mujibu wa Gavana, sekta ya nje imeendelea kuimarika kutokana na athari za janga la Uviko-19, ikiendelea kuwa na nakisi ndogo za urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamishaji mali nchi za nje.

Alifafanua katika taarifa hiyo kuwa, hali hiyo inatokana na kuanza kuingia mapato ya nje ya mauzo ya madini, mazao ya biashara na shughuli za utalii.

Gavana Luoga alisema kwa kuzingatia tathimini ya mwenendo wa uchumi wa hivi karibuni na matarajio ya mfumuko wa bei kuendelea kubaki ndani ya lengo, Kamati ya Sera ya Fedha imeridhia BoT kuendelea kutekeleza sera ya fedha inayolenga kuongeza ukwasi kwa kipindi cha Novemba na Desemba, mwaka huu ili kuendelea kuimarisha uchumi.

Na WILLIAM SHECHAMBO

Previous Post

MIHANJI AHIMIZA USHIRIKIANO WA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI

Next Post

PM ATAKA WENYE ULEMAVU WAPEWE FURSA VIWANDANI

admin

admin

Next Post
PM ATAKA WENYE ULEMAVU WAPEWE FURSA VIWANDANI

PM ATAKA WENYE ULEMAVU WAPEWE FURSA VIWANDANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Instagram Youtube Twitter Facebook

Browse by Category

  • ! Без рубрики
  • 1
  • 2
  • 231
  • Afya Makala
  • autohenriquesevale.pt
  • best casino
  • Best online casino
  • BIASHARA
  • BURUDANI
  • Business
  • Casino
  • Casino No Deposit Bonus
  • Casino UK
  • casino1
  • casino2
  • casino3
  • casino4
  • curapractic-kerpen.de
  • Forex News
  • gambling platform
  • gambling platforms
  • Gry
  • gry hazardowe
  • HABARI KIMATAIFA
  • Habari Kitaifa
  • Habari Picha
  • Kasyno Polska
  • KIMATAIFA
  • MAGAZETI
  • MAHAKAMANI
  • MAKALA
  • MAKALA AFYA
  • MAKALA-BURUDANI
  • mew casino
  • MICHEZO
  • MICHEZO KIMATAIFA
  • MICHEZO KITAIFA
  • MICHEZO-MAKALA
  • MICHEZO-MASUMBWI
  • MITINDO
  • Nasi Partnerzy
  • new casino
  • niam.cl
  • non gamstop casinos
  • Nos partenaires
  • OM cc
  • Online Casino
  • Online Kasyno
  • Our Partners
  • Partners
  • Post
  • Pozyczki
  • Prestamos
  • Public
  • ready_text
  • RIWAYA
  • sanodelucas.cl
  • SIASA
  • Slots
  • Sports
  • test
  • The best new online casino
  • The best online casino and sportsbook
  • UK Casino
  • Uncategorized
  • Unsere Partner
  • veterinariarepublica.cl
  • wildbeauty.cl
  • www.kuss.cl
  • Микрокредит
  • Наши Партнеры

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved

No Result
View All Result

© 2020 Uhuru Media Group. All rights reserved